Burna Boy achukizwa na picha yake ambayo hana ndevu

Staa wa muziki kutoka Nigeria,Burna Boy ameonyesha kukasirishwa na kitendo mtandao wa The Shaderoom kutoka nchini Marekani kutumia picha yake za mwaka 2021 ambayo hakuwa na ndevu.

Mkali huyo amekiri kuwa alinyoa ndevu zake mwaka 2021 na sio hivi karibuni kama inavyodaiwa na baadhi ya mitandao ya kijamii.

Kauli ya Burna Boy imezua mjadala mpana kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya watumiaji wakimuunga mkono kwa kusisitiza umuhimu wa kuzingatia mafanikio ya wasanii badala ya habari binafsi, wakati wengine wakimkosoa kwa kile wanachokiita kutothamini maoni ya mashabiki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *