Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema Bunge limepitisha bajeti kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2023/2024 kwa kupiga kura 354 sawa na asilimi 95
Dkt. Tulia ameyasema hayo Leo Juni 26, 2023 wakati akitangaza matokeo ya kura hizo ambapo amesema wabunge waliokuwepo Leo Bungeni ni 374 na wasiokuwepo 18
Dkt. Tulia amesema waliopiga kura za ndio ni 354 kura zisizo za uamuzi (Abstain) ni 20 na kura za hapana ni 0.