Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Bunda:Waiomba Serikali Kumuondoa Mvamizi wa Ardhi

Na Adam Msafiri,Mara

Wananchi katika kijiji cha Mekomariro wilayani Bunda mkoani Mara,wameiomba serikali kumuondoa mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Magambo Makori,anayedaiwa kuvamia eneo lililotengwa na kijiji hicho kwa ajili ya shughuli za malisho ya mifugo.

Wakizungumza na Jambo Media Septemba 9,2024 Bw.James Mboyi,Bhoke Mwita na Nyamwabe Mkono ambao ni miongoni mwa wakazi wa kijiji hicho,wamesema walitenga eneo la malisho tangu miaka ya 90 lakini ghafla alitokea mtu huyo  na kuweka makazi huku akizuia wananchi kufika wala kupita katika eneo hilo.

“Mwenyekiti unashindwa kabisa kumtoa Magambo kwenye eneo la kijiji anasababisha migogoro,kila leo migogoro watu wanapigana mishale watu wanakufa,tunazika watu kwa ajili ya mtu mmoja” Amesema Nyamwabe Mkono mmoja wa wakazi wa kijiji Mekomariro.

Jambo Media ililazimika kumtafuta kwa njia ya simu malalamikiwa kwa njia ya simu ambapo amesema kuwa mgogoro uliopo ni kati ya kijiji na kijiji na sio baina yake na kijiji kama inavyoeleza,ambapo pia amesisitiza kuwa kama angelikuwa na mgogoro na wanakijiji hao basi walipaswa  kufungu kesi mahakamani.

“Wao ndio wanashindwa kukueleza ukweli kwa sababu wao ndio wamefanya mambo mengi,mgogoro uliopo pale ni wa kijiji na kijiji na sio baina yangu na kijiji hicho,na kama ni hivyo kwamba nimechukua haki yako wangeenda mahakamani”Ameeleza Bw.Magambo

Kufuatia sakata hilo,serikali ya mkoani  Mara kupitia kwa Mkuu wa mkoa huo Kanali Evans Mtambi,amesema kuwa wamejiridhisha kuwa mtu huyo anayelalamikiwa na wananchi,aliingia katika eneo hilo bila kufuata utaratibu na hivyo tayari serikali imeagiza apishe katika eneo hilo la malisho ya mifugo.

Kanali Mtambi Amesema wumejiridhisha kwamba kwa utaratibu huo,wale wananchi waliongia kwenye eneo na kubadilisha matumizi basi hawapaswi kuwa katika eneo hilo,kwa hiyo kamati ya usalama imeagiza kwamba zifuatwe taratibu za kisheria za kuwaondoa wananchi hao ambao wameingia kwenye eneo lililokuwa limetengwa na kijiji cha Mekomariro kwa ajili ya malisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *