BUMBULI WAAHIDI KWENDA NA SAMIA, WAMTAKA MAKAMBA TENA

Wananchi katika Jimbo la Bumbuli linaloongozwa na Mhe. Januari Makamba, wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia miradi ya kimaendeleo kupitia Mbunge huyo, ikiwemo Umeme, Maji na Zahanati.

Wakiongea kwa nyakati tofauti, Wananchi hao wamesema Bumbuli ya mwaka 2010 sio ile inayoonekana hivi leo, kwani wamepiga hatua kubwa na kumepata maendeleo ambayo yamefanikishwa kwa usimamizi wa Mbunge wao Januari Makamba.

“Tumefanya tathmini, hakuna mtu wa kukutoa hapa. Ubunge labda uache wewe mwenyewe tu, lakini Bumbuli ya mwaka 2010 sio Bumbuli ya leo. Tumepata maendeleo makubwa sana.”

Hata hivyo, pamoja na kusifu maendeleo hayo, Wananchi hao pia wamemtahadharisha Mbunge Makamba uwepo wa fitna kwani huu ni mwaka wa uchaguzi na kwamba wana imani Makamba atashinda tena kwa kishindo.

”Huu ni msimu wa siasa na tumeshaanza kuona dalili za fitina, yaani watu wa huko nyika, ambao hawakai Bumbuli na hawajui Bumbuli ilikuwaje huko nyuma, ndio wameshikia kidedea mambo ya Bumbuli, Watuache na Mbunge wetu utazisikia kwamba hufai lakini sisi tutakufa na wewe na utashinda kwa kishindo na Mama Samia atashinda kwa kishindo pia.” walisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *