BONDIA MWINGINE WA TANZANIA AFARIKI BAADA YA KUPIGWA TKO….

BONDIA wa ngumi za kulipwa Tanzania, Hassan Mgaya, amefariki dunia usiku wa Desemba 29 muda mchache baada ya kupewa rufaa ya kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoka Hospitali ya Mwananyamala na Palestina aliyopelekwa awali.

Chanzo cha Kifo cha bondia huyo kimesababishwa na kupigwa ngumi nyingi za kichwa katika raundi ya tano na mpinzani wake Paul Elias kabla ya kuanguka kisha kung’ata ulimi kuzama, katika pambano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Dunia Ndogo, Tandale jijini Dar es Salaam siku ya  jana Jumamosi Desemba 27, 2024

Mweka Hazina wa Chama cha Mabondia, Cosmas Cheka amesema kuwa Mgaya amepatwa na umauti wakiwa katika harakati za kumuhamisha kwenda Muhimbili kutokana na hali yake kubadilika baada ya mchana wa leo Desemba 28, 2024 kupelekwa Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza, kisha Mwananyamala.

Baada ya tukio hilo, alipatiwa huduma ya kwanza na kurejea katika hali yake ya kawaida ambapo asubuhi ya leo Jumapili hali ilibadilika na kukimbizwa hospitali. 

Bondia huyo anakuwa wa pili kufariki dunia hapa nchini kwa siku za karibuni baada ya pambano kufuatia mwezi uliopita mchezo wa ngumi kumpoteza bondia Abbasi Mselem aliyefariki kufuatiwa kupigwa katika pambano lake Zanzibar.

Chanzo: Mwanaspoti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *