Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Bondia Mandonga kupimwa Afya yake

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imesema bondia wa ngumi za kulipwa, Karim Mandonga hatoshiriki ngumi mpaka atakapopimwa afya yake baada ya kupigwa TKO katika pambano lake na Moses Golola kutoka Uganda lililofanyika Julai 29, 2023 jijini Mwanza.

Katibu wa TPBRC, George Lukindo amesema Mandonga anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi Agosti 15 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na majibu ya uchunguzi ndiyo yatatoa majibu endapo ataruhusiwa kucheza pambano lake litakalofanyika Agosti 27 mwaka huu visiwani Zanzibar.


Kwa mujibu wa Lukindo Mandonga amefungiwa mpaka Septemba 13 mwaka huu na mpaka sasa hakuna dalili yoyote mbaya ambayo ameionesha ya kiafya baada ya pambano jijini Mwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *