Bondia Issa Simba akisha namba mbili kwa Ubora

Bondia matata kanda ya ziwa kutoka Manispaa ya Kahama, Shinyanga, Issa Salum James [Issa Simba], amepanda viwango na kuwa bondia namba pili Tanzania kwenye uzito wa Super lightweight, nyuma ya kinara Tony Rashid wa Dar es salaam.

Simba ambaye ni bingwa wa kimataifa wa UBO na WABA, Kwa mujibu wa Boxrec bondia huyo ana rekodi ya kucheza mapambano matatu [3], akishinda yote kwa TKO na KO.

Pambano lake la mwisho alicheza Julai 15 mwaka jana uwanja wa taifa Kahama, dhidi ya Limbani Chikapa na kuibuka na ushindi wa TKO raundi ya 9 akiutetea mkanda wake wa UBO International.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *