Boda Boda kutoka wilayani Korogwe mkoani Tanga, wamechoma moto basi la abiria la kampuni ya Sai Baba baada ya mwenzao kugongwa na basi hilo jirani na shule ya sekondari Semkiwa katika Kata ya Mtonga halmashauri ya wilaya ya Korogwe Mjini na kudaiwa kufariki.
Kamishna Msaidizi wa Polisi mkoani humo, Almachius Mchunguzi amesema kijana huyo amefariki dunia na dereva wa basi anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.