
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko leo Januari 22, 20204 ameongoza mapokezi ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong ambaye yupo nchini kwa ziara ya Siku tatu.
Akiwa nchini, Mhe. Guozhong anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa