BILIONI 26.5 ZA SAMIA KUWAFARIJI WAFANYABIASHARA SIMIYU

Na Saada Almasi – Simiyu.

Wananchi wa Mkoa wa Simiyu, awamepata faraja ya kunufaika na biashara, mara baada ya kushuhudia utiaji saini baina ya Mkandarasi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wenye thamani ya shilingi Bilioni 26.5 kwa ajili ya ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa Wilayani hapo.

Akizungumza na Jambo Fm baada ya utiaji saini, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoani humo, Hamka Nyanda amesema haikuwa rahisi kwa Wafanyabiashara kuvumilia kipindi kirefu tangu wahamishwe eneo lao la kazi, lakini kwa sasa wanauona mwanzo mpya.

“Tangu mwezi wa tisa mwaka jana wapo wafanyabiashara ambao mitaji iliyumba,wengine walikimbiliakwenye magulio wengine mitaji ilikuwa lakini sasa tunaona mwanzo mpya ombi letu ni kukamilikwa kwa wakati,” amesema Nyanda.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, aamemtaka Mkandarasi kutumia Wafanyabiashara wa ndani ya mji kumsambazia vifaa vya ujenzi, huku akitoa angalizo kwa Wafanyabiashara wenye tabia ya kupandisha bei ya bidhaa zao.

Amesema, “mmepigiwa chapuo na mheshimiwa Mbunge Kundo hapa kuwa bidhaa zinunuliwe hapa, lakini niwambie hatutomlazimisha Mkandarasi kukunua bidhaa kwenu kama mmepandisha bei makusudi kwa kuwa mnajua kuna bilioni 26, hiyo kasumba mnayo bidhaa mtakazo muuzia mkandarasi zilingane na bei halali.”

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bariadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Andrea amewaambia Wananchi hao kuwa baada ya kukaa na Wafanyabiashara hao mwaka 2021 walimuomba ujenzi wa soko hilo na baada ya kuomba bungeni fedha zilitoka na sasa anafarijika kuona tamati ya kilio chao.

Amesema, “nilikaa na hawa wananchi mwaka 2021 wanaomba soko lijengwe niliomba fedha za kujenga soko la kawaida lakini baada ya mpango wa kujenga masoko ya kisasa katika miji mikubwa kutufikia nikaomba kujengewa soko la kisasa mjini hapa japo ni mkoa mchanga lakini nikaidhinishiwa na sasa pesa zimekuja ujenzi unaanza.”

Akitoa taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Idd Ndabona amesema kiasi hicho cha Fedha, pia kitatumika kujenga Barabara 13 za mji huo pamoja na Barabara viunganishi zenye urefu wa kilometa 1.4, ujenzi ambao utatekelezwa na Mkandarasi Harisson Mchau, ukitarajiwa kukamilika Novemba 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *