Bilioni 14 za nunua vifaa tiba

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo Januari 5, 2023 amezindua ugawaji wa vifaa tiba vitakavyo sambazwa katika majimbo yote 214 katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo katika kila Halmashauri itafaidika na mgao huo.

Waziri Ummy amesema Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya Tsh. Bilioni 14 mwezi November 2023 na kununuliwa vifaa hivyo ili kuendelea kuboresha huduma za Afya ya uzazi, mama na mtoto.

Miongoni mwa vifaa ambavyo Waziri Ummy amepokea ni pamoja na vitanda vya wagonjwa 3,080, vitanda vya kujifungulia 1,000, magodoro 5,500, mashuka 36,808, pamoja na meza za vutanda 306.

Aidha, Waziri Ummy amesema takwimu zinaonesha asilimia 86 ya wanawake wajawazito Tanzania wanajingulia katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali za Halmashauri, vifaa hivyo vitakwenda kusaidia kuboresha huduma za Afya ya uzazi, mama na mtoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *