Bilioni 13 kujenga kituo kipya cha kisasa

Kutokana na changamoto ya kukosa Kituo cha kisasa cha Mabasi Serikali Mkoani Geita, imetenga zaidi ya Bilioni 13 kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya cha kisasa kitakachojengwa katika eneo la msitu wa Usindakwe Halmashauri ya mji wa Geita.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Zahara Michuzi ambapo amesema kituo hicho kipya kitasaidia kukuza mji wa Geita pamoja na kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wakazi wa Mkoa huo.

Mhandisi wa halmashauri ya Mji wa Geita Osward Mtei amesema ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kuanza Disemba 2023 ambapo kwa sasa wapo katika hatua za manunuzi pamoja na mkandarasi ambaye atatekeleza ujenzi wa mradi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *