Bilionea Elon Musk amefunguliwa mastaka na mpenzi wake wa zamani Claire Boucher, ‘Grimes’ kwa kutopewa haki ya kulea watoto wake watatu ambao wamezaa.
Bi Grime amefanya hivyo kwa kuwasilisha ombi lake Mahakama ya Juu ya San Francisco, kutaka Bilionea huyo kumpa nafasi aweze kulea watoto wake kwani amemfungia hawezi kulea watoto hao ambao ni Æ A-1, anayejulikana kama X, ambaye alizaliwa Mei 2020, na binti anayeitwa Exa Dark Sideræl – anayejulikana kama Y – ambaye alipatikana kwa njia ya mtoto kuzaliwa na mwanamke mwingine mnamo Desemba 2021, Techno Mechanicus, au Tau, alizaliwa Juni mwaka jana.
Kwa mujibu wa rekodi za mahakama zinaonyesha kwamba Grimes, aliwasilisha ombi la malezi ya watoto mnamo 29 Septemba na Bw Musk ana takriban watoto 11 na wanawake watatu tofauti.