Bila  dola  biashara ya mafuta hatutoboi

Katika kuendelea kuhakikisha bidhaa ya mafuta ya petroli inapatikana kwa uhakika maeneo yote nchini, Chama cha Waagizaji na Wasambazaji mafuta Tanzania (TAOMAC) wamekutana na Waziri wa Nishati, January Makamba katika Ofisi ndogo za Wizara Ya Nishati Jijini Dar Es Salaam.

Katika kikao hicho, TAOMAC wametoa taarifa ya mwenendo wa biashara ya mafuta Duniani  hapa nchini pamoja na kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya mafuta hususani suala la upatikanaji wa dola za marekani ambapo wamesema  uhaba wa dola za Marekani katika soko la fedha unapelekea waagizaji kupunguza kiasi cha mafuta wanayoagiza kuepuka kuagiza mzigo na kushindwa kuulipia kwa wakati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *