Biden Aipa Booster Ukraine Kuikabili Urusi

Rais wa Marekani Joe Biden ameipa Ukraine idhini ya muda kutumia silaha za Marekani kushambulia ndani ya Urusi kwa lengo la kutetea mji wa Kharkiv.

Haya yameelezwa na maafisa wawili wa Marekani wanaofahamu suala hilo kwa sharti la majina yao kutotajwa na wamesisitiza kuwa sera ya Marekani inayoitaka Ukraine kutotumia makombora yake ya masafa marefu pamoja na zana nyingine kushambulia ndani ya Urusi bado haijabadilika.

Awali Uamuzi huo wa Biden uliripotiwa na shirika la habari la Marekani, Politico na hatua hiyo inakuja katika wakati ambao maafisa wa Ukraine wameimarisha wito kwa utawala wa Marekani kuruhusu vikosi vyake kujilinda dhidi ya mashambulizi kutoka eneo la Urusi.

Maafisa wa Ukraine, haswa Rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelensky wamekuwa wakisema kuwa vizuizi vya kutotumia silaha za magharibi dhidi ya Urusi vinaviweka vikosi vya nchi hiyo katika hali ngumu wakati Urusi ikizidisha mashambulizi katika eneo la kaskazini mashariki la Kharkiv.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *