Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Bibi amchoma moto mjukuu wake kisa karanga za mboga

Mtoto anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 7 ameunguzwa mikono yote miwili na bibi yake aliyetambulika kwa jina la Vestina Edward mkazi wa mtaa wa Uwanja kata ya Nyankumbu wilaya na Mkoa wa Geita akimtuhumu kudokoa karanga za kuungia mboga.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Uwanja Enos Cherehani amesema baada ya kupata taarifa za tukio hilo alifika eneo la tukio n akukuta mtoto huyo ameunguzwa moto na alipomhoji mtoto huyo alisema ameunguzwa na bibi yake .

Mtuhumiwa wa tukio hilo Vestina Edward ambaye ni bibi wa mtoto huyo amekiri kufanya kitendo hicho huku akisema alifanya hivyo kwa lengo la kumkanya kuacha tabia ya udokozi.

Baadhi mashuhuda wa tukio hilo ambao ni wakazi wa mtaa huo wamekemea kitendo hicho huku wakitaka hatu kali za kisheria zichukuliwe ili iwe fundisho kwa wazazi na walezi wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *