Staa wa muziki, Beyonce na bintiye Blue Ivy Carter wanaweka historia ya kuwa mama na mwana wa kwanza kuigiza filamu ya ‘Mufasa’ The Lion King.

Filamu hiyo imeongzwa na Jon Favreau, na kwa mujibu wa Box Office katika siku ya kwanza ya uzinduzi wake imeingiza kiasi cha dola milioni 192.
Mwaka jana pia Blue Ivy aliingia kwenye jukwaa la ziara ya Renaissance na mama yake na wawili hao mpaka sasa tayari wana tuzo ya Grammy ya video bora ya muziki waliyoipata kupitia wimbo wa Brown Skin Girl.


