Ifikapo Machi 29,2024 staa wa muziki kutoka Marekani Beyoncé anatarajia kuachia albamu yake mpya iitwayo “Cowboy Carter”, amesthibitisha hilo kupitia Ukurasa wake wa Instagram
Ujio wa albamu hii umesubiriwa kwa hamu na mashabiki wake, kwani alionesha balaa kwenye albamu yake iliyopita “Renaissance” ambayo ilitikisa chati mbalimbali za muziki duniani.
Jina la albamu “Cowboy Carter” limezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki, wengi wakionekana kushangazwa na uteuzi wa jina hilo.