BESIGYE AGOMA KULA AKIHOFIA USALAMA WAKE GEREZANI

Kiongozi wa upinzani Nchini Uganda, Dkt. Kizza Besigye amegoma kula akiwa Gereza la Luzira jijini Kampala, akipinga kuendelea kushikiliwa huku akisema anahofia usalama wa maisha yake.

Dkt. Besigye alikamatwa mwaka jana 2024 Nchini Kenya na mekuwa kizuizini toka kipindi hicho, na ameshitakiwa kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria, kuchochea vurugu na uhaini.

Dkt. Besigye amesema anahisi yuko hatarini kwani mlalamikaji wake ni Serikali ambaye pia ana mamlaka ya udhibiti wa Gereza na kwamba ana.hofu ya kuwekewa sumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *