Na Saulo Stephen – Singida.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida, Bertha Nakomolwa amekutana na makundi mbalimbali ya watu katika wilaya ya Ikungi Mkoani humo kwa lengo la kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaibuka na ushindi katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akiwa wilayani Ikungi, Nakomolwa ametembelea Kata ya Ingelason, Kitongoji cha Nkurusi, huku akiongozana na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Wazazi akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa singida.

Miongoni mwa Makundi waliyoyatembelea ni pamoja na wajasiriamali mbalimbali lakini pia ametembelea kaya kwa kaya ambapo wameyaleza Makundi hayo kuhusu ilani ya CCM 2020-2025 ilivyotekelezwa na chama hicho na kuyaomba Makundi hayo kukiamini tena chama hicho katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu ili watekeleze zaidi ilani hiyo kwa mwaka 2025-2030.
Aidha Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Singida ameyaomba Makundi hayo kuwachagua Madiwani wa CCM, Wabunge pamoja na Mgombea urais wa chama hicho Dkt.Samia Suluhu Hassan.


