Wakati Kendrick Lamar akifunga onesho lake kwa wimbo wake wa “Tv off,” Mwanamume mmoja aliyevalia nguo nyeusi alipanda juu ya gari na kupeperusha bendera ya Palestina baada ya kukimbia kuzunguka jukwaa.
Mtu huyo ambaye baadaye alikuja kugundulika kuwa ni Mwandamanaji, alisimama juu ya gari jeusi ambalo Lamar alifungua onesho lake na kuelekea kwenye mstari wa yadi 50 kabla ya kukabiliwa na watu wa usalama.

Bado hijabainika mara moja iwapo Mwanamume huyo ambaye aliiandika bendera hiyo majina ya SUDAN na GAZA kama alikuwa ni sehemu ya onesho la Lamar, ambalo lilijumuisha makumi ya wachezaji waliovalia mavazi sawa.

Hata hivyo, Mwandamanaji huyo alikamatwa na kufungwa pingu na kisha kusindikizwa nje ya uwanja na maafisa wa usalama wasiopungua watano.
Onesho hilo, pia lilihudhuriwa na ma Star kibao akiwemo Serena Williams aliyeonekana jukwaani wakati wa onyesho hilo la Super Bowl Half Time Show, akiwa na SZA, Mustard na Samuel L. Jackson.