Bei Ya Saa Ya Abiria Tajiri Wa Titanic, Yavunja Rekodi

Saa ya dhahabu iliyovaliwa na abiria tajiri zaidi kwenye Titanic bwana John Jacob Astor IV,imeuzwa mara sita zaidi ya bei iliyokuwa ikiuzwa awali, na imenunuliwa kwa dola milioni $1,46 sawa na Bil. 3.7 za Kitanzania.


Saa hiyo iliuzwa jumamosi na kampuni ya mnada ya Henry Aldridge & Sonna mnada huo ulifanyika huko Devizes, Wiltshire, Kusini Magharibi mwa Uingereza ambapo inaelezwa kuwa ni kama imevunja rekodi ya dunia.
Yani ni bidhaa iliyozwa kwa pesa ya juu kutoka kwenye vituo mbalimbali vilivyopatikana kwenye meli ya Titanic.


Saa hiyo ilikuwa ya John Jacob Astor IV, mfanyabiashara na msanidi programu wa majengo ambaye alishuka na meli hiyo ilipozama katika Bahari ya Atlantiki mwaka wa 1912.
Titanic ilizama mapema Aprili 15, 1912, baada ya kugonga jiwe la barafu katika Bahari ya Atlantiki Kaskazini ikiwa takriban watu 1,500 wanaaminika kufariki kutokana na tukio hilo.
So kama unataka kutazama tukio la meli ya titanic basi itafute filamu ya Titanic iliyotoka Desemba 19, 1997.
Filamu hiyo imeongozwa na James Cameron na imeigizwa na Leonardo DiCaprio kama Jack Dawson na Kate Winslet kama Rose DeWitt Bukater.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *