Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Bei ya Mbolea ya ruzuku kujulikana leo

Rais Samia Suluhu Hassan leo anatarajiwa kuzindua bei elekezi ya ruzuku ya mbolea kwa wakulima kwa msimu mpya wa kilimo.

Anatarajiwa kuyafanya hayo wakati anafunga maonesho ya wakulima (nanenane) kitaifa katika Viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.

Wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa maonesho hayo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Serikali inafanya juhudi ikiwa ni pamoja na kuishirikisha sekta binafsi na kuweka bei elekezi ili wakulima wanufaike. Pia alisema leo utafanywa uzinduzi mwonekano wa viwanja vya maonesho ya kimataifa ya kilimo vya Mbeya na Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *