Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Bei ya mafuta yazidi kushuka

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) leo Jumatano Januari 3, 2023 imetangaza bei mpya za mafuta ambazo zimeshuka ikilinganishwa na mwezi uliopita.

Bei ya mafuta ya petroli imeshuka kutoka Sh 3,158 Desemba 2023 hadi Sh 3,084 Januari 2024 katika Mkoa wa Dar es Salaam, huku ya dizeli ikishuka kutoka Sh 3,226 hadi Sh3,078 katika kipindi kama hicho.

Mbali na Mkoa wa Dar es Salaam pia bei za mafuta ya petroli pia imeshuka katika Mikoa ya Tanga na Mtwara ambavyo ndiyo vitovu vya kupokelea mafuta hayo.

Taarifa Iliyotolewa Na Ewura imesema Kupungua kwa bei za mafuta kwa Januari 2024 ni kwa sababu ya kushuka kwa bei za mafuta (FOB) katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 6.03 kwa petroli na asilimia 7.13 kwa dizeli.

Aidha Taarifa Hiyo imeongeza kuwa kupungua kwa bei za mafuta kumetokana na kushuka kwa gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 3.72 kwa petroli na asilimia 17.52 kwa dizeli kwa bandari ya Dar es Salaam na kwa wastani wa asilimia 22.71 kwa petroli na asilimia 22.12 kwa dizeli kwa bandari ya Mtwara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *