Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta zilizoanza kutumika leo Novemba 1, ambapo kwa mafuta yanayoshukia bandari ya Dar Es Salaam, petroli ni tsh. 3,274, dizeli tsh. 3,374 na mafuta ya taa tsh. 3,423.
Tanga, petroli ni tsh. 3,274 kutoka tsh. 3,327, dizeli imepanda kutoka tsh. 3,494 hadi tsh. 3,510, mafuta ya taa yamepanda hadi tsh. 3,469 kutoka tsh. 2,989. Mtwara, petroli itauzwa tsh. 3,347, dizeli tsh. 3,546 na mafuta ya taa yamepanda hadi tsh. 3,495 kutoka tsh. 3,016.
Licha ya mabadiliko ya kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kwa wastani wa 5.68% na gharama za uagizaji wa petroli kwa 13%, dizeli 25%, bei za mafuta nchini bado hazijaonesha unafuu kwa watumiaji.