Koti la ngozi lililovaliwa na Michael Jackson mwaka 1984 limenunuliwa kwa $306,000 sawa na zaidi ya TSh. Milioni 764 huko nchini Uingereza Ijumaa iliyopita. Koti hilo lenye rangi nyeusi na nyeupe, lilivaliwa na mwimbaji huyo katika tangazo la kinywaji baridi.
Koti hilo ni moja ya bidhaa 200 za kumbukumbu za muziki zilizouzwa London siku ya Ijumaa, ikiwa ni pamoja na koti la George Michael na sehemu ya nywele za Amy Winehouse.
Kwa bei ya koti hilo unaweza nunua ndinga za maana nyingi na ukafanya na ujenzi wa nyumba zako mwaya!!