Baraza la Sanaa la Taifa @basata.tanzania limetoa onyo kali kwa wasanii wote kuacha tabia ya kujirekodi au ku-rekodiwa na kusambaza picha au video zisizo na maadili kwenye mitandao ya kijamii kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kanuni za uendeshaji wa shughuli za sanaa na maadili ya kitanzania.
Aidha BASATA limeongeza kuwa halitasita kuchukua hatua kali ikiwemo kufutiwa leseni na kibali cha kujishughulisha na kazi ya sanaa kwa wote watakaoenda kinyume na tamko hilo kwani itatafsiriwa kuwa ni uvunjaji wa sheria.