
Barcelona imekataa ofa ya Euro milioni 60 kutoka kwa klabu ambayo haijatajwa inayotoka katika Ligi kuu ya Uingereza iliyoweka mezani kiasi hicho kwa lengo la kumnunua Raphinha .
Winga huyo amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Xavi Hernandez katika siku za hivi karibuni, hasa akifunga bao la mwisho dhidi ya Las Palmas na mabao mawili na kuisaidia Barcelona kupata faida ya 3-2 katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Paris Saint-Germain katika mechi ya kwanza ya hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Vilabu vingi vya Ulaya vimekuwa vikimtazama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 lakini Barcelona wameamua kwamba hawatakubali chochote chini ya Euro milioni 80.

Pia Barca inafahamu wanafahamu uwezo wa kifedha ambao vilabu vya juu vya kuu ya Uingereza vinao na wanahisi kwamba wanapaswa kutoa ofa kubwa kwa mchezaji wa ubora wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, huku Manchester United na Chelsea zikitajwa kuwa huenda zikafika dau linalohitajika na Barcelona ili kumuachia mchezaji huyo ambaye amewahi kuitumikia klabu ya Leeds United inayoshiriki katika Ligi kuu ya Uingereza.