BARABARA ZOTE SHINYANGA KUWEKWA LAMI

Na Gideon Gregory – Dodoma.

Serikali imesema itaenda kujenga barabara ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyaga kwa kiwango cha lami kwasababu mpango wao ni kuwa katika maeneo yote ya makao makuu ya Wilaya au Halmashauri ni kuwa barabara zote zinakuwa na lami.

Hayo yameelezwa leo Februari 6,2025 Bungeni hapa Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Dkt. Christina Mzava aliyehoji ni lini Serikali itaweza angalau kuwajengea mita chache ya kipande cha lami katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

“Kwahiyo nimuhakikishie Mhe. Mbunge kuwa tutalichukua na tutalifanyia kazi ikiwa ni pamoja na ombi la RCC kuunganisha mji wa Shinyanga na Halmashauri ya Shinyanga DC,” amesema.

Aidha akizungumzia kuhusu ujenzi wa barabara Old Shinyanga hadi Solwa Mha. Kasekenya amesema kuwa wamekwisha kupokea maombi rasmi ya mkoa kwa maana kwamba wafikishe barabara hiyo mpaka makao makuu.

Wakati huo huo Mha. Kasekenya amemuakikishia Mbunge wa Nyang’hwale Mhe. Hussein Amar na wananchi wake kuwa wanategemea mwezi wa Tatu mwaka huu mshauri mwelekezi atakuwa site kwaajili ya kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwaajili ya ujenzi wa barabara inayounganisha Wilaya Tatu za Kahama, Nyang’hwale na Busisi – Sengerema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *