Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Bangili zilizochukuliwa na Wajerumani mwaka 1884 zimeomba kurudishwa nchini

Moja kati ya vitu ambavyo kwasasa vinaoneka kusahaulika ni tamaduni na vitu vya kale kutokana na utandawazi uliopo, moja kati ya tukio ambalo limewashangaza wengi ni kuhusiana na Bangili ambayo ilichukuliwa na Wajerumani miaka kadhaa iliyopita ambapo kwasasa imegeuka kuwa mzigo kwao kutokana na usumbufu wa mara kwa mara wa bangili hizo kuomba kurudishwa nchini.

Akizungumza na Jambo Chief wa Kabila la Wagogo Lazaro Chihoma wa Himaya ya Bwibwi amesema Wajerumani walichukua Bangili hiyo kwa kudhani kuwa ni uchawi wa kuwafanya washindwe kutimiza walichokua wakihitaji kufanya kwa waati huo.

Nao baadhi ya wananchi walioshiriki kwenye tambiko hilo Wameeleza shauku waliyonayo ya kuipokea bangili hiyo huku wakiamini kuwa mambo mengi yaliyoshindikana kutatulika kwa kipindi cha muda mrefu sasa yanakwenda kupata ufumbuzi kupitia bangili hizo.

Vitu vya kitamaduni vilivyochukuliwa na nchi za Magharibi kwasasa vinaanza kurudishwa ikiwemo Bangili iliyochukuliwa kwa kabila la wagogo Wakati wa utawala wa Wajerumani mwaka 1884.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *