BANGI ZAWAFIKISHA POLISI WATUHUMIWA 12 SINGIDA

Na Saulo Stephen – Singida.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida limeendelea kuonesha mafanikio katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya baada ya kuwakamata jumla ya watuhumiwa 12 katika operesheni maalum zilizofanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa Singida, SACP Amon Kakwale ameeleza kuwa watuhumiwa saba walikamatwa wakiwa na bangi yenye uzito wa gramu 7,548, ikionyesha ukubwa wa mtandao wa biashara hiyo haramu unaoendelea kudhibitiwa.

SACP. Amon Kakwale.

Aidha, watuhumiwa wengine watano walinaswa wakiwa na pombe haramu aina ya moshi yenye ujazo wa lita 23, ambayo nayo imekuwa ikiathiri afya za watumiaji pamoja na kuvuruga maadili ya jamii.

Kamanda Kakwale amebainisha kuwa hatua kali za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao ili kuhakikisha wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria,huku akionya kuwa hawatasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na biashara au usambazaji wa dawa za kulevya katika mkoa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *