Balozi wa Zambia nchini Afrika Kusini amefutwa kazi na Rais wa Zambia kwa utovu wa nidhamu, Rais Hakainde Hichilema wa Zambia amechukua uamuzi huo baada ya Balozi Baalizi Mazuba Monze, kuripotiwa kutaka wafanyakazi wake wa kiume kumnyoa sehemu zake za siri.
Mwanadiplomasia huyo ambaye alikuwa akifanya kazi katika ubalozi wa Zambia mjini Pretoria ameripotiwa kutoa ombi hilo lisilo la kawaida, Balozi Mazuba anatajwa kuwataka wafanyakazi wa Ubalozini kumnyoa sehemu zake za siri ambapo wafanyakazi hao walikataa, wakisema kuwa haikuwa sehemu ya majukumu yao kumnyoa balozi hasa sehemu za siri.
Balozi Mazuba alichukulia kitendo hicho kama sehemu ya kutotii maelekezo yake na hivyo kupelekea kuwafuta kazi Wafanyakazi, hata hivyo baada ya ukimya wa muda mrefu wafanyakazi walikata rufaa dhidi ya uamuzi huo na kulifikisha suala hilo kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wakati madai kuhusu matakwa hayo yaliyoshangaza wengi ya Monze yalipothibitishwa, Rais Hakainde Hichilema alimfuta kazi mara moja balozi huyo wakati huo huo ripoti nyingine zinasema kuwa madai dhidi ya Monze yametiwa chumvi.