Bado wanakimbiza YouTube

Wiki hii tunakutana tena kwenye chati ya Youtube on Trending, kwa muziki wa Bongo Flava ambapo nafasi zimepanda na kushuka.

Namba 1: Jux Ft Diamond Platnumz– Enjoy

Wiki iliyopita alikuwa Zuchu ameshika nafasi ya kwanza na Honey, ila wiki hii ni video ya Enjoy kutoka kwa Jux ft Diamond Platnumz, video imetoka siku tano zilizopita na inawazamaji Milioni 2.3 na ni #1 on Trending for music.

Namba 2: Zuchu – Honey

Honey, ya Zuchu inazidi kupenya kila sehemu na wiki hii kashika nafasi ya pili kutoka ya kwanza wiki iliyopita. Mpaka sasa Honey, inawatazamaji Milioni 4.1 kwa wiki mbili zote ilivyotoka na ipo #2 on Trending for music.

Namba 3: Alikiba- Mnyama

Hii ni ngoma kwaajili ya klabu ya Simba SC, imetoka siku tisa zilizopita na inawatazamaji Milioni 1.6 . Awali nafasi hii ilikuwa ikishikwa na Jux Ft Diamond Platnumz – Enjoy.

Namba 4: Lava Lava a ft Diamond Platnumz- Kikao.

Hapa Konde anatolewa anaingia Lava Lava Ft Diamond Platnumz – Tuna Kikao. Video ya ngoma hiyo imetoka siku tatu zilizopita na inawatazamaji laki 509.

Namba 5: Harmonize- Tena

Marioo Feat. AliKiba – Love Song, inatolewa kwenye nafasi hii na Harmonize – Tena, ngoma hii ya mapenzi imetoka siku 10 zilizopita na inawatazamaji Milioni 1.2.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *