Babu Tale amsifia Isarito

Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na Meneja wa Diamond Platnumz Babu Tale amempa maua yake Muigizaji wa filamu Isarito kutokana na uwezo wake wa kuigiza.

Babu Tale amempongeza Isarito kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika ujumbe wa kumsifia mugizaji huyo kutokana na kazi yake ya Sanaa anayofanya.

“Leo nimechuma maua yenye Oksijeni ya pongezi
nyingi Juu ya Kijana Mwenye juhudi ziliandikwa kwa
mpango wa jasho.

Acha leo nimpe mauwa yake huyu mwamba japokuwa mimi sijawahi kumuona uso kwa uso, ila nimejikuta tu nakuwa Shabiki yake kwa kile anachokifanya kwenye kila kazi yake yake ya Sinema.

Ndugu yangu @isarito_tmt najua unajua kuwa Mimi
sikujui hata chembe, lakini nataka ufahamu kuwa, Mimi ni Shabiki yako namba moja kwa sasa.
Naomba upige kifua chako na jue kuwa, Wewe ni
Mkali haswaa na nakuona mbali sana katika safari ya heshima na mafanikio.

Kikubwa endelea kusimamia kile ambacho Mungu amekupa kwani naamini lazima kitatoa matunda kwako, familia yako na Nchi kwa ujumla.
Endelea kukaza kwakuwa jasho la haki ya kazi yako litakulipa thamani ya heshima itakayoishi vizazi na vizazi”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *