Na Afarah Suleiman Babati – Manyara.
Kikundi cha Wanawake cha Self Love cha Wilayani Babati Mkoani Manyara, kimeshiriki michezo ya kirafiki na timu ya Wanawake ya Tanzanite ya Wilaya humo, yenye lengo la kuhamasisha Wananchi ikiwemo Wanawake wenzao, kujitokeza kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025.
Mgeni Rasmi kwenye michezo hiyo ambaye ni mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emanuela kaganda, Ismail Kashaha amewapongeza Wanawake hao kwa ushirikiano walioungesha na kusisitiza umuhimu wa kupiga kura kwa maendeleo ya wilaya hiyo, mkoa na Taifa kwa ujumla.

Aidha, Kashasha ameiopongeza kampuni ya Duttchkona kwa kuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na jamii kwenye mambo mbalimbali ikiwemo kudhamini mashindano hayo, pamoja na ujenzi wa vyoo katika shule Sekondari ya Komoto iliyopo wilayani Babati.
Awali akisoma Risala, Mratibu wa mashindo hayo Esther Chessa, amesema lengo la kuandaa ni kuwaweka Wanawake pamoja katika kushirikiana kwenye mambo mbalambili ya kijamii na kiuchumi, ikiwemo ushiriki katika kupiga kura.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mdhamini mkuu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Duttchkona kupitia kinywaji chake cha Jogoo na kisungura, Noreen Mollely amesema wamefurahishwa na wazo la Wanawake wa Self Love na kuhaidi kuendelea kuwashika mkono wwao na makundi mengine.