BABA WA NEYMAR AMALIZA UVUMI WA MWANAYE KUREJEA BARCA

Baba mzazi wa nyota wa Soka Neymar Jr. amemaliza uvumi unaoenea kuhusu uwezekano wa mwanasoka huyo kurejea Klabu ya soka ya Barcelona akisema mwanawe amejitolea kikamilifu kuihudumia klabu iliyomlea ya Santos.

Hatua ya mzazi wa Neymar kuongea hayo inatokana na uvumi uliosambaa kuwa Mbrazil huyo (33) huenda akarejea Uhispania ingawa madai hayo pia yalikanushwa na Neymar Mwenyewe.

Mapema hivi karibuni, Neymar alisherehekea kurejea kwa kiwango chake kwa kuifungia Santos bao lake la kwanza la alilolipata kwa penati, toka Oktoba 3, 2023 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Agua Santa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *