Baba mzazi wa Mohbad, Joseph Aloba, ametoa tamko juu ya vipimo vya DNA vya mjukuu wake, Liam anayetajwa kuwa ni mtoto wa promota Sam Larry ambaye anatajwa kuhisika na mauaji ya msanii Mohbad
Akizungumza na kwenye mahojiano na BBC Pidgin mzee Aloba, amesema “Jambo hili limekuwa jambo la wengi, sio Nigeria pekee. Kwa hiyo wanapaswa kufanya jambo linalofaa kwa wakati ufaao.” Hii ni baada ya kuulizwa na matangazaji kuwa anafahamu kinachoendela mtandaoni juu ya mashabiki wa marehemu mtoto wake wakitaka DNA ya mtoto wa Mohbad.
Ikumbukwe kuwa bado majibu ya chanzo cha kifo cha Mohbad
hayajatoka tangu Jeshi la Polisi Nigeria kufukua mwili wa msanii huyo.