Staa wa Muziki kutoka Nigeria, Davido amesema kuwa hakuwa na mpango wa kukishtaki kituo cha habari cha K 24 cha nchini Kenya kwa kumzushia kukamatwa na dawa za kulevya ndani ya ndege yake binafsi akiwa katika ziara ya kikazi.
Davido alilazimika kufanya hivyo kwa kuwa baba yake alimwambia kwamba habari hiyo ingemletea shida kwasababu yeye (Davido) anasafiri sana hivyo Polisi na vikosi vya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya wangekuwa wanamuwinda kila wakati katika viwanja vya ndege.
Taarifa za Davido kukamatwa akiwa nchini Kenya zilisambaa baada ya kituo cha habari cha K24 kuandika kwamba msanii huyo amekamatwa baada ya kukutwa na dawa za kulevya kwenye ndege yake binafsi iliyotua nchini humo wikiendi ya sikukuu ya Pasaka, hata hivyo Davido alikanusha taarifa hizo zilitolewa April Mosi ambayo imekuwa ikitajwa kuwa ni siku ya wajinga duniani!