Hamis Said (37), mkazi wa Mtaa wa Nkokoto mjini Igunga anashikiliwa na polisi kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kufanya mapenzi na kumpa ujauzito binti yake mwenye umri wa miaka 16.
Akizungumza na gazeti la #mwananchi , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema binti huyo (jina linahifadhiwa) ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika moja ya shule za sekondari wilayani Igunga ambaye jina lake linahifadhiwa kutokana na umri wake.
Bila kuelezea kwa kina tukio hilo lilivyogundulika hadi mtuhumiwa kutiwa mbaroni, Kamanda Abwao amesema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na kinakiuka maadili, mila na desturi.
Ameiomba jamii kukemea vitendo vya aina hiyo huku akiwasihi wenye taarifa za matukio ya namna hiyo kutoa taarifa kwa vyombo vya dola au viongozi wa Serikali katika maeneo yao kuwezesha hatua za kisheria dhidi ya wahusika.