Baada ya wiki za mzozo, uchaguzi wa urais Senegal kufanyika Machi 24

Rais wa Senegal Macky Sall ametangaza kwamba duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais itafanyika Machi 24, baada ya wiki za mgogoro mkubwa na uamuzi wa Baraza la Katiba kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi baada ya mwisho wa muhula wake Aprili 2.

Baraza la Katiba pia lilikataa pendekezo lingine lililotolewa kwa Rais Sall na kutangaza kuwa orodha ya wagombea 19 ambayo tayari imethibitishwa na taasisi hiyo isifanyiwe marekebisho.

Ofisi ya rais wa Senegal imebaini uharakishaji huu wa ghafla wa kalenda kwa kutangaza jioni kwamba Waziri Mkuu Amadou Ba ameondolewa kwenye wadhifa wake kwa minajili ya kuongoza kampeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *