
Bilionea na msanii wa muziki Rihanna usiku wa jana alikuwa miongoni mwa wahudhuriaji wa hafla ya maonyesho ya Fenty X Puma, ambayo yamefanyika Jijini London, Uingereza na alikutana na msanii wa muziki kutoka Nigeria Ayra Starr.

Wawili hao walikuwa kwenye mazungumzo ya muda mrefu kidogo jambo linalotafirisiwa kuwa huenda walikuwa wakifanya mazungumzo ya kikazi.
Mwaka 2021, Mwezi Septemba Rihanna alikutana na Tems na wawili hao walifanikiwa kufanya kazi pamoja ambayo ni ‘Lift Me UP’ ngoma ambayo ilitumika kwenye filamu ya Wakanda na kuwania tuzo kubwa za muziki.
