
Klabu ya Manchester United imeamua kukifuta cheo cha Ukurugenzi wa michezo baada ya kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Nottingham Forest kwenye uwanja waOld Trafford, Jumamosi iliyopita.
Mmiliki wa klabu hiyo, Sir Jim Ratcliffe amemfuta kazi Dan Ashworth ikiwa ni miezi mitano tu toka apewe nafasi hiyo mpya huku sababu ikitajwa ni matokeo mabovu ya mechi iliyopita, Kwa sasa Dan Ashworth amekuwa kwenye mawindo ya klabu ya Arsenal ikitaka huduma yake.
Bilionea Ratcliffe ameamua msaidizi wake kwenye kampuni ya Ineos, Sir Dave Brailsford kuwa mkurugenzi mtendaji mkuu wa Man United, Omar Berrada na mkurugenzi wa ufundi, Jason Wilcox watagawana majukumu yaliyokuwa yakifanywa na mkurugenzi wa michezo.


