Klabu ya Fountain Gate imetangaza kulivunja benchi lake lote la ufundi baada ya matokeo ya leo ya kufungwa 5 – 0 na Yanga kwenye uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge Jijini DSM.
Taarifa iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Fountain Gate imesema ‘Uongozi wa timu yetu ya Fountain Gate Football Club umeamua kulivunja benchi lote la fundi lilokuwa likiongozwa na kocha wetu mkuu Mohamed Muya. Klabu inawashukuru kwa mchango wao ndani ya timu na kuwatakia kila la kheri’ – Afisa Mtendaji Mkuu.
Sababu za kuvunjwa benchi hili la ufundi hazijawekwa wazi lakini inaonyesha imechangiwa na mwenendo mbovu wa timu hii kwenye mechi kadhaa ambazo imecheza.