Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Baada ya kuchanganya maiti ,Muhimbili kutoa ufafanuzi

Uongozi wa Hospitali ya Muhimbili, umeahidi kutoa ufafanuzi leo, Oktoba 20, 2023 baada ya kutokea kwa tukio la kuchanganya maiti ambapo mwili wa marehemu Emanuel Ngowo ulikabidhiwa kimakosa kwa ndugu wa marehemu mwingine kisha kusafirishwa.

Marehemu Ngowo ambaye mwili wake ulipaswa kusafirishwa kwenda Moshi kwa mazishi, ulisafirishwa kwenda Songea mkoani Ruvuma na kuzua taharuki kwa ndugu baada ya kubaini kuwa hakuwa ndugu yao waliyemtarajia.

Wakati huohuo, familia ya Ngowo imeeleza kuwa inasubiri mwili wa ndugu yao kurudishwa kutoka Songea kwa ndege kisha waanze safari ya kuelekea Moshi.

“Ni kweli tukio limetokea hapa hospitalini kwetu, tumeliona na tumeanza kuchukua hatua kadhaa, undani wa tukio tutazungumza na wanahabari…” amesema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *