Umewahi kujiuliza binadamu aliyehai anaweza kuishi ndani ya kaburi la futi sita kwa siku saba?, sasa kutana na mwanamitandao, MrBeast ambaye ameamua kujirecord video akiwa amezikwa hai kwa siku saba.
Katika video yake ya ‘I Spent 7 Days Buried Alive’, MrBeast, ameonyesha akiwa anazikwa kwenye kaburi la futi sita na anaweka nia ya kukaa humo kwa siku saba na akiwa kwenye jeneza hilo ataendelea na Maisha yake ila akiwa amelala tu.
Akiwa kwenye jeneza hilo, pia anaelezea namna atakavyoishi kwa siku saba kwa kuonyesha vitafunwa na vinywaji. Ila ndani ya siku nne tu hali yake kila mara ikiwa haipo sawa na alikuwa akihisi uchovu sana siku ya nne na akasema hakuweza kulala.
Mpaka sasa video yake imefikisha zaidi ya watazamaji 64,279,371 na anafanikiwa kumaliza siku saba ambapo anataka na kuonekana ametimiza nia yake huku akiwa ameongeza wafuasi wengi zaidi katika channel yake ya Youtube.