AZAM WAMEMALIZANA NA YANNICK BANGALA??

Azam FC huenda ikaachana na mchezaji wake raia wa DR Kongo, Yannick Litombo Bangala, aliyekuwa amebaki na mkataba wa miezi michache klabuni hapo kabla ya kumalizika.

Bangala ambaye alijiunga na Azam mwezi Julai 2023 akitokea Klabu ya Yanga, alisaini mkataba wa miaka miwili ambao ulipaswa kumuweka Azam hadi Julai 30 2025.

Kwa sasa miezi nane imebaki kabla ya kuisha kwa mkataba wake na zipo taarifa zinasema Azam imeamua kumvunjia mkataba na kumlipa fidia ya muda uliobakia.

Taarifa zisizo rasmi kutoka kwa watu wa karibu na Bangala zinadai Azam imemlipa zaidi ya Shilingi Milioni 100 za Tanzania ili kufidia mkataba huo.

Taarifa hizo zinasema baada ya mechi ya Tabora, wakala wa Bangala alipigiwa simu na uongozi wa klabu kumwambia wameamua kuachana naye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *