Aweso apewa wiki 3 kukamilisha mradi wa maji

Katibu wa NEC Itikadi, uenezi na mafunzo Paul Makonda amemtaka Waziri wa Maji Juma Aweso kuhakikisha ndani ya wiki tatu kuanzia leo Novemba 11 2023 awe amekamilisha mradi wa Maji katika Mji mdogo wa Katoro uliopo wilaya na Mkoa wa Geita ili kumaliza changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji ya kutosha kwa wakazi mamlaka hiyo.

Akizungumza kwa njia ya Simu waziri wa Maji Juma Aweso amesema serikali kupitia Wizara ya Maji inatekeleza mradi wa maji katika Mji huo wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 6.5 ambapo kwa sasa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 92 na ndani ya Mda huo mradi huo utakuwa umekamilika ili wananchi waanze kupata huduma ya maji.

Waziri Aweso amesema ili kumaliza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama Katika Mkoa wa Geita serikali inatekeleza pia mradi mkubwa wa maji wa miji 28 ikiwemo mikoa wa Geita ambapo mpaka kufikia 2025 mradi huo utakua umekamilika na kumaliza kabisa kero ya Maji katika Mkoa wa Geita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *