Mrembo kutoka Nigeria, Helen William ameingia kwenye Rekodi ya Dunia ya Guinness ya kutengeneza wigi refu zaidi kwa kutumia mikono yake.
Guinness wametoa taarifa ya mrembo huyo kuingia kwenye rekodi hiyo siku ya siku ya Jumanne,(Jana)
Helen, ametumia siku 11 na kiasi cha zaidi ya naira milioni mbili sawa na Tsh/= 6,310,077.90 kutengeneza wigi lake lenye urefu wa mita 351.28.
Mrembo huyo kutoka Nigeria amekuwa akifanya kazi kama mtaalamu wa kutengeneza wigi kwa miaka minane, na amekuwa akitengeneza wigi 50 hadi 300 kwa wiki.