Mzee wa miaka 60 Abdul Sambuka ameuawa kwa kushambuliwa na watu wenye hasira baada ya kuhutumiwa kumbaka mtoto wa miaka mitano katika Kijiji cha Nyamambaya Wilaya ya Urambo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao amethibitisha tukio hilo huku akidai marehemu alimvizia mtoto huyo nyumbani kwao ambako anaishi na bibi yake.
Mpaka sasa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na jeshi la polisi kwa kumuua mzee huyo na uchunguzi unaendelea ili kubaini aliyehusika ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.