Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Aua mtoto kwa kumtumbukiza kwenye ndoo ya maji

Johari Mbuma (19) mkazi wa manispaa ya Iringa anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Iringa kwa tuhuma za kumtumbukiza mtoto wake wa miezi saba kwenye ndoo yenye maji na kumsababishia kifo na yeye kutoweka.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mawelewele kata ya Mwangata Obedi Mtatifikolo amesema taarifa za tukio hilo ziliripotiwa Novemba 19, 2023 na Wakazi wanaoishi kwenye nyumba ambayo choo chake kilikutwa mtoto akiwa ametumbukizwa kwenye ndoo huku kichwa kikiwa chini miguu juu.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, Mama wa mtoto huyo amekamatwa asubuhi ya Novemba 20, 2023 baada ya kuonekana akirandaranda eneo la tukio ambalo watu walikusanyika kushangaa ukatili huo uliofanywa kwa kichanga hicho.

Alipohojiwa na Mwandishi wa TBC mkoani Iringa Johari amesema, alichukua uamuzi wa kumdumbukiza mtoto kwenye ndoo baada ya kuona anachekwa na wenzake huku ndugu zake wakimsimanga.

Choo alichotumia kumtumbukiza mtoto wake ni cha nyumbani kwa rafiki yake ambaye alikwenda kumsalimia lakini hakumkuta na yeye kuamua kuingia kujisaidia na kutenda kitendo hicho.

Jeshi la Polisi mkoani Iringa linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo na litatoa taarifa mara baada ya upelelezi kukamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *